WHAT IS CRYPTOCURRENCY
tunaita ulimwengu wa cryptocurrency kwani ndiko kwa sasa ulimwengu unabadilika kwa kasi kwa maana ya technology kuelekea huko. Hapa utaweza kujifunza cryptocurrency kwa ujumla pia utapata nafasi ya kujifunza jinsi gani unaweza kutengeneza kipato chako enedelevu kupitia biashara hii ya cryptocurrency tofauti na fursa/biashara zingine za online.. pia ningependa kukuhakikishia kuwa usalama wa pesa zako uko guaranteed yaani wa uhakika ila endapo utazidisha umakini juu ya details zako za account zako kwani huku hakuna mtu anashika pesa zako kwani kila kitu unakuwa nacho wewe mwenyewe kwenye acount yako either kwa simu au computer yako or other device..
MAELEZO KUHUSU CRYPTOCURRENCY
Cryptocurrency ni mfumo mpya wa kifedha ambao tunaweza kuuita ni mfumo wa kidigital kwani haina hii ya fedha au sarafu/coins huwezi kuzishika kw mkono wala kuziona kwa macho kama zilivo pesa za kawaida na pia hata katka usafiri wake baina ya mtu mmoja na mwingine hufanyika kwa njia ya mtandao tu tena katika mfumo wake imara na wenye ulinzi wa kutosha ujulikanao kama BLOCKCHAIN.
Kwa kuongezea CRYPTO -nikitu chochote kinacho onekana na kinathamani lakini hakiwezi kushikika (You can see it but cant touch it)
CURRENCY -ni Sarafu kama inavyojieleza mfano; dollar,tanzania tshs,Pound n.k
Hivyo kwa Ujumla Crypto currency ni sarafu zenye thamani kama sarafu zingine na zinaonekana lakini huwezi kuzishika kwa mikono
Nadhani hapo tuko pamoja umepata concept kamili ya Crypto currency
Sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa biashara ya  Crypto currency
Kwanini cyptocurrency ilitengenezwa? lliundwa baada ya kuyumba kwa uchumi wa dunia mnamo mwaka 2008 kama njia mbadala ya watu kuwa na mamlaka na pesa zao wenyewe, bila kutegemea kampuni, benki, au serikali kusimamia au kushikilia pesa zao. Hivyo unatakiwa kuelewa kua iliundwa ili kila mtu awe benki.
Baaadhi ya changamoto zinazoikumba cryptocurrency. 1.Elimu na uelewa juu ya cryptocurrency Tatizo hili ni kubwa sana kwani ni watu wachache sana wana uelewa japo kidogo juu ya mifumo hii ya kimitandao na pia kama tunavyoona hapa hii mifumo yote inajiendesha na kufanya kazi online ni watanzania wachache sana wana elimu au uelewa juu ya cryptocurrency na hata mitandao kwa ujumla na tunashindwa kuelewa tupo kwenye.. "Information Age" hivyo ruka au lala "Internet is a Fuel" Uchumi na kipato cha kweli kipo mtandaoni.
2.Utapeli Yani hii ni changamoto kubwa sana kwenye ili soko kwani kuna utapeli wa hali ya juu na hiyo inatokana na kwamba kwa kua elimu juu ya cryptocurrency bado haijapenya kwa upana wake wanaojua uhalisia wake ni watu wachache sana.. hivyo wengine wanatumia hiyo fursa kutapeli. Mfano; kuna baadhi ya watu wanatengeneza kampuni kabisa na kutapeli watu na wanafunga kampuni wanapotea na pesa za watu. Ni muhimu sana ujifunze kwa undani mambo haya kabla hujafanya maamuzi ya kuweka pesa zako. UTALIA!
3.Watu Kutaka pesa za haraka na kwa pupa (Tamaa) Hili ni tatzo ni kubwa sana miongoni mwa vijana wengi wa Tanzania na Africa kwa ujumla, utakuta kijana akishapata uelewa kidogo juu ya bitcoin anaanza kutafuta sehemu ya kuwekeza kwa haraka pasipokuwa na uhakika juu ya usalama wa kampuni hiyo ila anawekeza kwasababu tu ameambiwa inalipa vizuri na yeye anataka pesa za haraka.. mwisho wa siku anajikuta kampuni hiyo inapotea mtandaoni na anakula hasara na baadae na yeye anaanza kuamini kuwa cryptocurrency ni utapeli au wizi na baadae anakata tamaa juu ya crptocurrency na kuwathibitishia watu wa jamii inayomzunguka kuwa cryptocurrency sio salama, kumbe yeye ndio alikurupuka na kufanya maamuzi yasiyo sahii pia hakupata uelewa wa kutosha juu ya fursa hii.
4.Mitizamo hasi juu ya cryptocurrency Mfano;- kuna watu hata ukijaribu kuwaelezea maana tu ya bitcoin ni nini na inafanyaje kazi, wao moja kwa moja wanajua ni wizi na wanakwambia hiyo ni DECI, wao wanaamini kuwa bitcoin au cryptocurrency ni kikundi cha watu fulani wamekaa.. na kuunda kitu fulani kwaajili ya kuiba pesa za watu kitu ambacho sio kweli. Lakini tunatakiwa tujue hakuna kitu ambacho hakina utapeli hata kuna makanisa ambayo kazi yao kubwa ni kutapeli watu hivyo ni vizuri kuchunguza jambo kwa undani kabisa kabla ya kufanya maamuzi ya kuweka PESA zako.
Have you checked out https://exonumia.africa/, they are doing translations into african languages, you can also help if you have the time
reply
I have also follow you twitter @tanzaniasats and in Damus ✊🏿⚡️🇹🇿
reply
Let me check now thanks a lot brother
reply