WHAT IS CRYPTOCURRENCY
tunaita ulimwengu wa cryptocurrency kwani ndiko kwa sasa ulimwengu unabadilika kwa kasi kwa maana ya technology kuelekea huko. Hapa utaweza kujifunza cryptocurrency kwa ujumla pia utapata nafasi ya kujifunza jinsi gani unaweza kutengeneza kipato chako enedelevu kupitia biashara hii ya cryptocurrency tofauti na fursa/biashara zingine za online.. pia ningependa kukuhakikishia kuwa usalama wa pesa zako uko guaranteed yaani wa uhakika ila endapo utazidisha umakini juu ya details zako za account zako kwani huku hakuna mtu anashika pesa zako kwani kila kitu unakuwa nacho wewe mwenyewe kwenye acount yako either kwa simu au computer yako or other device..
MAELEZO KUHUSU CRYPTOCURRENCY
Cryptocurrency ni mfumo mpya wa kifedha ambao tunaweza kuuita ni mfumo wa kidigital kwani haina hii ya fedha au sarafu/coins huwezi kuzishika kw mkono wala kuziona kwa macho kama zilivo pesa za kawaida na pia hata katka usafiri wake baina ya mtu mmoja na mwingine hufanyika kwa njia ya mtandao tu tena katika mfumo wake imara na wenye ulinzi wa kutosha ujulikanao kama BLOCKCHAIN.
Kwa kuongezea
CRYPTO -nikitu chochote kinacho onekana na kinathamani lakini hakiwezi kushikika (You can see it but cant touch it)
CURRENCY -ni Sarafu kama inavyojieleza mfano; dollar,tanzania tshs,Pound n.k
Hivyo kwa Ujumla Crypto currency ni sarafu zenye thamani kama sarafu zingine na zinaonekana lakini huwezi kuzishika kwa mikono
Nadhani hapo tuko pamoja umepata concept kamili ya Crypto currency
Sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa biashara ya Crypto currency
Kwanini cyptocurrency ilitengenezwa?
lliundwa baada ya kuyumba kwa uchumi wa dunia
mnamo mwaka 2008 kama njia mbadala ya watu
kuwa na mamlaka na pesa zao wenyewe, bila
kutegemea kampuni, benki, au serikali kusimamia
au kushikilia pesa zao.
Hivyo unatakiwa kuelewa kua iliundwa ili kila mtu
awe benki.
Baaadhi ya changamoto zinazoikumba
cryptocurrency.
1.Elimu na uelewa juu ya cryptocurrency
Tatizo hili ni kubwa sana kwani ni watu wachache
sana wana uelewa japo kidogo juu ya mifumo hii ya
kimitandao na pia kama tunavyoona hapa hii
mifumo yote inajiendesha na kufanya kazi online
ni watanzania wachache sana wana elimu au
uelewa juu ya cryptocurrency na hata mitandao kwa
ujumla na tunashindwa kuelewa tupo kwenye..
"Information Age" hivyo ruka au lala "Internet is a
Fuel" Uchumi na kipato cha kweli kipo mtandaoni.
2.Utapeli
Yani hii ni changamoto kubwa sana kwenye ili
soko kwani kuna utapeli wa hali ya juu na hiyo
inatokana na kwamba kwa kua elimu juu ya
cryptocurrency bado haijapenya kwa upana wake
wanaojua uhalisia wake ni watu wachache sana..
hivyo wengine wanatumia hiyo fursa kutapeli.
Mfano; kuna baadhi ya watu wanatengeneza
kampuni kabisa na kutapeli watu na wanafunga
kampuni wanapotea na pesa za watu.
Ni muhimu sana ujifunze kwa undani mambo haya
kabla hujafanya maamuzi ya kuweka pesa zako.
UTALIA!
3.Watu Kutaka pesa za haraka na kwa pupa
(Tamaa)
Hili ni tatzo ni kubwa sana miongoni mwa vijana
wengi wa Tanzania na Africa kwa ujumla, utakuta
kijana akishapata uelewa kidogo juu ya bitcoin
anaanza kutafuta sehemu ya kuwekeza kwa haraka
pasipokuwa na uhakika juu ya usalama wa kampuni
hiyo ila anawekeza kwasababu tu ameambiwa
inalipa vizuri na yeye anataka pesa za haraka..
mwisho wa siku anajikuta kampuni hiyo inapotea
mtandaoni na anakula hasara na baadae na yeye
anaanza kuamini kuwa cryptocurrency ni utapeli au
wizi na baadae anakata tamaa juu ya crptocurrency
na kuwathibitishia watu wa jamii inayomzunguka
kuwa cryptocurrency sio salama, kumbe yeye ndio
alikurupuka na kufanya maamuzi yasiyo sahii pia
hakupata uelewa wa kutosha juu ya fursa hii.
4.Mitizamo hasi juu ya cryptocurrency
Mfano;- kuna watu hata ukijaribu kuwaelezea maana
tu ya bitcoin ni nini na inafanyaje kazi, wao moja kwa
moja wanajua ni wizi na wanakwambia hiyo ni
DECI, wao wanaamini kuwa bitcoin au
cryptocurrency ni kikundi cha watu fulani wamekaa..
na kuunda kitu fulani kwaajili ya kuiba pesa za watu
kitu ambacho sio kweli.
Lakini tunatakiwa tujue hakuna kitu ambacho
hakina utapeli hata kuna makanisa ambayo kazi yao
kubwa ni kutapeli watu hivyo ni vizuri kuchunguza
jambo kwa undani kabisa kabla ya kufanya maamuzi
ya kuweka PESA zako.